
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Rais wa lebo ya Sharobaro Records ya jijini Dar es Salaam, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kufunga pingu za maisha, kimwana anayetarajiwa kupika mahajumuti nyumbani kwa bosi huyo wa wasafi dunia nzima amejulikana.
Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo kimoja kilichopo mjini Zanzibar, kimeidokeza Teentz.com kuwa Bob Junior huenda akafunga pingu za maisha na nyota wa filamu kutoka visiwani humo Halima Ally ‘Imma’ ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa karibu kwa kiasi kikubwa na Produza huyo kila anaikanyaga ardhi ya visiwa hivyo vya karafuu.
“Hakuna mwingine ni Halima, siku zote Bob junior amekuwa akija huku na tunawaona wakitumia muda mwigi wakiwa pamoja hivyo ni uhakika kuwa Halima ndiye anayeolewa, na hapo kabla mwenyewe aliwahi kutuambia kuwa wakati wowote atakuwa mke wa mtu” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa kuna wakati mrembo huyo aliwahi kuishi nyumbani kwa akina Bob Junior kwa majuma kadhaa.
Halima alikuwa mmoja wa mastaa walioshiriki filamu ya Royal Prince iliyotayarishwa visiwani humo chini ya kampuni kubwa El- Fahad Production anatariwa kutambulishwa rasmi kama mke wa Bob Junior mbele ya mashabiki wakati bosi huyo wa Sharabaro atakapokuwa anafanya uzinduzi wa albamu yake ndani ya Club Billicannas jijini Dar es Salaam.
STORI NA DISMAS TEN
Comment
Comment by abra da maybach jr on July 6, 2012 at 12:22pm kaka ni uamuzi mzuri uliochukua big up
Comment by Luparkiss on July 5, 2012 at 2:18am KAOPOA SHOMBESHOMBE KAMA YEYE SIO MBAYA.
Comment by BENNY DAUD on July 4, 2012 at 10:56pm ebwanae bob we mkaleeeeeeeeeeeee ichokifaa ningekuwa me sikipi chansi ya kutoka ata nje mwana bigup xana
Comment by abdallawaziri on July 4, 2012 at 11:42am
Comment by Hamady on July 4, 2012 at 9:48am
Comment by Noah Silungwe on July 3, 2012 at 5:52pm totoo ya ukweli kwa msanii wa ukweli,ebana daaaa kama vipi mpige kiss afu tusikie ile muaaaaaaaaah
Comment by CHE OSWARD on July 3, 2012 at 11:42am hiyo 100 bro,
Comment by Ersar mkude on July 2, 2012 at 1:49am
Comment by robert matunda on July 1, 2012 at 9:29pm baba shombeshombe mama ndo kama mnavyomuona mtoto cjui atakua mdhungu
sohel khan posted an album© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ