
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Rais wa lebo ya Sharobaro Records ya jijini Dar es Salaam, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kufunga pingu za maisha, kimwana anayetarajiwa kupika mahajumuti nyumbani kwa bosi huyo wa wasafi dunia nzima amejulikana.
Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo kimoja kilichopo mjini Zanzibar, kimeidokeza Teentz.com kuwa Bob Junior huenda akafunga pingu za maisha na nyota wa filamu kutoka visiwani humo Halima Ally ‘Imma’ ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa karibu kwa kiasi kikubwa na Produza huyo kila anaikanyaga ardhi ya visiwa hivyo vya karafuu.
“Hakuna mwingine ni Halima, siku zote Bob junior amekuwa akija huku na tunawaona wakitumia muda mwigi wakiwa pamoja hivyo ni uhakika kuwa Halima ndiye anayeolewa, na hapo kabla mwenyewe aliwahi kutuambia kuwa wakati wowote atakuwa mke wa mtu” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa kuna wakati mrembo huyo aliwahi kuishi nyumbani kwa akina Bob Junior kwa majuma kadhaa.
Halima alikuwa mmoja wa mastaa walioshiriki filamu ya Royal Prince iliyotayarishwa visiwani humo chini ya kampuni kubwa El- Fahad Production anatariwa kutambulishwa rasmi kama mke wa Bob Junior mbele ya mashabiki wakati bosi huyo wa Sharabaro atakapokuwa anafanya uzinduzi wa albamu yake ndani ya Club Billicannas jijini Dar es Salaam.
STORI NA DISMAS TEN
Comment
Comment by bob Gz on April 18, 2013 at 3:19pm katika wasnii wa bongo flava, ambao nimetoka kuapenda ni kama vile bob junio, diamond na ommy dpz
sema songeni mbele kwa vipaji mlivo pewa na mola
Comment by Alpha Mhagama on October 6, 2012 at 12:01pm cute
Comment by junior mkiza mchumaishoke on August 7, 2012 at 2:04pm jambo la kheri kuoa
Comment by johnson robben sugercane on August 6, 2012 at 2:20pm ni poa sana ila je wako tayari??????????
nakutakia maisha mema imma na bob
Comment by Allys Hance on August 2, 2012 at 3:29pm cha msingi ni kutulia kwenye ndoa tu....
Comment by andrew massawe on August 2, 2012 at 9:04am nipoa sana kaka
Comment by Mo Mocko on July 31, 2012 at 12:51am Kwa kuwa wote wako poa naamini watatulia. big up kwao
Comment by cuthbert mashauri on July 23, 2012 at 11:41pm apunguze majukumu yasiyo na msingi he started new lfe wth her wife
Inshallah M/mungu awaondolee shali na nuksi.
Hiphop staa wa Tanzania Albert Mangweha alifariki dunia akiwa Afrika Kusini May 28 2013 ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana na siku…
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ