
Miezi kadhaa baada ya kumtoa kumnawirisha kimuziki 'bwamdogo' Asley kutoka mitaa ya Temeke jijini Dar, kampuni kubwa ya muziki wa kizazi kipya Bongo, inayomiliki jina la 'Mkubwa na Wanawe' sasa iko tayari kumtoa mavumbini na kumvisha ustaa wa muziki nchini binti mdogo anayeitwa Asna Juma 'Ching Chilla'.
Akizungumza na Teentez.com muda mfupi uliopita 'Big Bos' wa kampuni hiyo Said Fella Mkubwa Fella amefunguka kuwa huu ni mwanzo wa mageuzi aliyopanga kuyafanya ndani ya muziki wa kizazi kipya kwa kuwatoa nyota wa k*** ambao walikuwa ama hawapewi nafasi sana kama ilivyo kwa vijana wa kiume.
"Kwa mara ya kwanza tunamtoa msanii mdogo wa k***, haya ni matunda ya mipango iliyopo katika kampuni yetu, kam ambavyo mnafahamu tumewatoa wengi lakini wote walikuwa ni wasanii wa kiume, safari hii tumeamua kuweka nguvu kwa wasanii wa k*** na tutahakikisha wanapata mafanikio kama ambavyo wanapata wasanii wa kiume, hivyo nawaomba wadau wamsapoti binti huyu ambae tumeanza naye ili kuweka chagizo kwa wasichana wengine kujitokeza na hatimaye tukapata wanamuziki wengi wa k*** wenye mafanikio kam ailivyo huko kwa wenzetu. alisema Fella.
hapa chini ni video ya wimbo mpya wa Ching Chilla so cheki nayo halafu utasema nayo
STORI NA DISMAS TEN
Comment
Comment by renatus dominick on July 31, 2012 at 10:17am Mkubwa na wanawe utaubeba mziki wa kibongo kwa kuwainua maandaground hapa bongo
Comment by ALLY YUSUPH on July 31, 2012 at 1:52am mtoto ni mkali, level za akina Mwacti, lyna. wimbo huu kuna sehemu alitakiwa kupanda sana, kunung'unika sana lkn hajafanya. kiwango alichoonyesha akizoea atakuwa mkali Bigup!
Added by tanjin tareq on May 18, 2013
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ