
Hiki ndiyo kichupa kipyaaa kutoka kwa mkali wa hip hop tz, Bonta, na muda mfupi kabla kideo hiki hakijang'aa hapa teentz mkali huyo alisema kuwa anajua jinsi gani ngoma hii inavyoleta sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya huku mijadala mikubwa ikiwa juu ya jila linalobeba wimbo huu lakini kwake yeye haimsumbui.
"Unajua mengi yanaweza kusemwa pale mtu unapoamua kufanya au kusema yaliyo ya kweli hilo halinisumbui sana kwa sababu nafahamu kuwa kwenye jamii yetu mtu anayesema ukweli anakuwa adui wa kila mtu na mtu muongo anapewa thamani kubwa kwangu mimi ukweli utabaki kuwa ukweli na sitaogopa chochote au kitakacho kuja nyuma yangu kwa sababu naamini ninachokisema wapo pia ambao kinawagusa lakini hawana mahali pa kupazia sauti zao jina la wimbo wangu litabaki kuwa hilo" alisema Bonta.
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ