
Unaweza usiamini lakini huu ndiyo ukweli, Siku chache baada ya kutua Bongo na kujiunga na kampuni ya Mtanashati Entertainments ya jijini, nyota wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ mwishoni mwa wiki iliyopita alisomea kisomo maalumu cha kuomba Mwenyezi Mungu amnyooshee mambo yake pindi atakapoanza kushusha ngoma mpya.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kisomo hicho kichoshudiwa na Teentz.com, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma alisema kuwa wameamua kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo janja mikononi mwa Mungu kwa kuwa wana amini wao watu ambao wajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo
.
“Ni wazi kuwa wapo watu ambao hawajafurahishwa na kurejea kwa Dogo Janja, na kama unavyojua binadamu wana hila zao ndiyo maana tumeamua kufanya kisomo hiki ili kila kazi yake iwe kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu” alisema Ostaz Juma na kuongeza kuwa tulichokifanya ni kwa ajili ya Mungu hivyo basi watu wasidili maneno na kusema tumefanya ‘ kafara’ alimaliza Ostaz.
Katika hatua nyingine baada ya kumalizika kwa kisomo hicho jana (Jumapili) Dogo janja alifanya ‘shopingi’ ya nguvu kwenye maduka makubwa ya viwalo yaliyopo Mlimani City jijini Dar.
Katika shopingi hiyo Dogo janja alitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5 za kibongo kununua vitu mbalimbali, kama Seti 5 za viatu, Suti 4, Jeans 10, T shirt 10,miwani 5, simu aina ya BlackBerry, Laptop na vitu vingine kibao .
Huku akionekana mwenye furaha kubwa Dogo Janja aliiambia Teentz.com kuwa amefuahi kwa kiasi kikubwa kwa yale yote ambayo Ostaz Juma na kundi zima la Mtanashati kwa yote wanayomfanyia hivi sasa kwani hatakuwa na malipo mengine zaidi ya kuwafanyia kazi nzuri zenye kiwango.
“Nina furaha sana, hakika namshukuru Ostaz kwa yote anayofanya kwangu sina la kusema zaidi wasubiri ngoma za kweli zitakazokuwa kama shukurani kwao kwa sababu ndiyo kitu pekee ambacho naweza kukifanya kwao” alisema Dogo Janja.
Comment
Comment by Donasian young barut lufega on June 30, 2012 at 12:04pm
Comment by Brian Gaitano Mlay on June 26, 2012 at 10:59pm dogo 2nakuomba 2lia na ufanye kweli na ucwe na bifu na kaka yako wa zaman kua kama una tatizo nae na mungu atakusaidia ila usahau kwamba kuna SHULE inakusubiri poa chalii 2lia na JUMA.....
Comment by Francis Kulwa on June 26, 2012 at 4:56pm ni muda wako dogo kutulia na kulipa fadhila kwa wote waliokusaport ili kukuza kipaji chako na kuwaonesha waliokudiss kuwa uaweza ndio maana mtanashati
Comment by khamis hk rais wa wachafu on June 26, 2012 at 3:59pm
Comment by kindururu on June 26, 2012 at 11:04am madee aache njaa njaa zake... sasa aibu kwake
Comment by samwel philipo mwanitete on June 26, 2012 at 12:14am piga kazi arifu kipaji unacho usibweteke
Comment by Tumaini Chanyika on June 26, 2012 at 12:04am
Comment by stephen mwanyonga on June 25, 2012 at 10:01pm sawa dogo,,, ila me nakusubiri studio nione cheche zako...........
Comment by Shanny Larry on June 25, 2012 at 8:00pm
Comment by issa waziri on June 25, 2012 at 6:52pm big up sana dogo nakukubali kinyama,ila kaza msuli class mbona hata raia wako tumeshaomba kabla ujaondoka kwa madee
Added by tanjin tareq on May 18, 2013
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ