TEEN TZ

DOGO JANJA ATUA JIJINI DAR, AJIUNGA MTANASHATI ENTERTAINMENT

Baadhi ya mashabiki wa Dogo Janja wakimsubiri Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.

..Mashabiki wakisubiri Dogo Janja awasili kutoka Arusha.

Dogo Janja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea jijini Arusha.

Dogo Janja akiwa kabebwa na mashabiki wake pamoja na baadhi ya wasanii wa kundi la Mtanashati.

Janja akiwa na PNC baada ya kuwasili jijini Dar.

PNC akibebwa baada ya kupoteza fahamu wakati wa shamra shamra za kumkaribisha Dogo Janja.

Mashabiki wa Dogo Janja wakiwa na mabango ya kumkaribisha.

Dogo Janja akiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya kundi la Mtanashati Entertainment.

Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja, leo amerudi jijini Dar es Salaam na kujiunga na kundi la Mtanashati Entertainment. Mwanzo Dogo Janja alikuwa kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha. Janja karudi jijini kwa ndege ya Air Tanzania na anataraji kusaini mkataba na kundi hilo la Mtanashati kuanzia sasa.

(PICHA ZOTE NA ERICK EVARIST/GPL)

Views: 1844

Tags: AJIUNGA, ATUA, DAR, DOGO, ENTERTAINMENT, JANJA, JIJINI, MTANASHATI

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by rajabu yusuph on June 27, 2012 at 12:07am

nafikili utulivu unahitajika la sivyo ataludi arusha 

Comment by Tumaini Chanyika on June 26, 2012 at 2:39pm

dah hii poa sana madee atulie kabisa..............

Comment by Kingu juma Ibrahim on June 25, 2012 at 7:12pm

soma dogo siku hizi elimu kwanza mengine baadae.

Comment by Idrissa Kefea on June 25, 2012 at 1:29pm

dogo komaa ila piga book  kwa sana

Comment by baraka samuel on June 24, 2012 at 3:19am

kaa ukijua kua hiyo ni second chance, kaza buti

Comment by Aloy Son Mlawa on June 24, 2012 at 12:45am

ametisha sana, madee kajipalia makaa

Comment by Mzee Shaban on June 23, 2012 at 11:04am

BABUUU Dogo sasa fanya kazi na hao vijana wenzako na pia utunze heshima kwa MADEE kwani kwanza ni kaka yako na pili amejitahidi kwenye part ya maisha yako.sisi wazee wako huku NGARENARO tunategemea utafanya kwani popote pale ukiwa na heshima utathaminiwa pia ukiwa na shida usisite kuomba ushauri kwa waliokutangulia katika fani hiyo.

 

Comment by Francis Kulwa on June 23, 2012 at 9:35am

sio siri binafsi nampongeza dogo janjaroooooooo kwa maujanjarooooooooooo ya pini zake, welcome back dogo, ila uwe makini, mjini hapaaaaaa

Comment by Haji Rashid on June 23, 2012 at 5:07am
Unajua kila cku maisha yanabadilika,ningemshauli dogo km ameamua kufanya mziki na si kusoma bac akaze ili mungu akimjalia hapo baadae arudi shule.
Comment by Gullam Mohammed Rashid on June 23, 2012 at 3:40am

dogo bongo mti mkavu mwana,, soma huku ukiendeleza kipaji,, utajuta baadae mdogo angu ooohhoooo we haya weeee

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service