TEEN TZ

FIESTA 2012 UWANJA WA SAMORA IRINGA ILIVYOCHUKUA NAFASI

Lina mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na Tausi mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa ambapo wasanii mbalimbali wanafanya vitu vyao jukwaani wakiburudisha mashabiki wa mkoa wa Iringa, Lina ameweza kufanya mambo makubwa na kuwaimbisha mashabiki wake ukizingatia kwamba anatoka mkoa huo

Meneja Masoko wa kampuni mya Push Mobile Rugambo Rodney akitangaza washindi wawili wa pikipiki walioshinda habati nasibu hiyo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Iringa kwenye uwanja wa Samora  huku wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongofleva wakionyesha uwezo wao katika muziki na kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika kwenye uwanja huo, katika picha aliyeshika kipaza sauti ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds B12

Amini akiimba jukwaani katika tamasha hilo

Mkali wa muziki wa R&B Ben Paul akikamua jukwaani  kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Msanii Rich Mavoko akiwa ameruka hewani wakati akicheza pamoja na wanenguaji wake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Iringa.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex akiimba kwa hisia kali jukwaani katika onesho la muziki la Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa , msanii huyo mwenye uwezo wa kutawala jukwaa amefanikiwa kukata kiu ya mashabiki wa muziki wake

Shabiki  wa muziki wa bongofleva anayejulikana kwa jina la Tausi akicheza  na rafiki yake  vilivyo  katika tamasha hilo.

 

Views: 636

Tags: 2012, FIESTA, ILIVYOCHUKUA, IRINGA, NAFASI, SAMORA, UWANJA, WA

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by chama-baby on September 25, 2012 at 2:46pm

kul

Comment by Toto mbata Lee on September 24, 2012 at 6:04pm

9c

Comment by erick kikanja on September 24, 2012 at 12:35pm

daa! baraaaaaaaaaaaaaaaaaaa

G5 CLICK - LATEST NEWS

Video za utengenezaji wa video ya mwisho aliyoonekana Marehemu Ngwea South Africa.

Hiphop staa wa Tanzania Albert Mangweha alifariki dunia akiwa Afrika Kusini May 28 2013 ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana na siku…


TOP PHOTOS

1. Agnes gerad

Added by Sekion Joseph on July 9, 2012

2. 4.u

Added by Rita on June 16, 2012

3. Agnes Masogange

Added by Sekion Joseph on November 11, 2012

 

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service