TEEN TZ

Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye nyota mwenye sauti ya zege kutoka tasnia ya muziki wa kizazi kipya Bongo Ismail kipira 'Ismail' amesema atakuwa tayari kuwashika mashabiki wake kwa mara nyingine mapema mwezi ujao.

Akizungumzana Teentz.com via 4n muda mfupi uliopita Ismail anayeitumikia bendi maarufu jijini iliyopewa jina la Mjomba Band amearifu kuwa ameamua kusitisha kwa muda ujio wake huo mpya kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani na pindi mfungo utakapomalizika atakuwa tayari kuitoa ngoma yake mpya iliyopewa jina la 'Mama Mwimbe' ambayo anaamini kuwa itamrudisha upya kwenye utawala wa muziki hapa Bongo.

"Ndiyo, hiyo itakuwa ngoma yangu mpya, imepikwa na Lamar, nimeamua kuipa jina hilo kwa kuwa iko kwenye mahadhi ya African Pop, nina imani kubwa kuwa itanirudisha kwenye utawala wa muziki wetu kama ilivyokuwa siku za nyuma" alisema Ismail

katika hatua nyingine nyota huyo amesema kuwa yuko kwenye mipango ya kufanya ngoma na wasanii kadhaa wa nje ikiwa ni pamoja nyota kutoka Kenya, Wyre na mkali kutoka DR Congo, Fally Ipupa ambaye tayari wameshaanza kufanya mawasiliano ya awali.

STORI NA DISMAS TEN 0718489260

Views: 230

Tags: 8, ISMAIL, KUTOKA, MWEZI, UPYA, WA

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by mansour shaweji on July 16, 2012 at 9:40pm

2na msubili hyo jombaaaa

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service