TEEN TZ

MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha mkoa wa Mbeya Izzo B,amesema kuwa Ijumaa hii inayokuja video ya ngoma yake ya ‘Utarudishwa’ itakuwa sokoni katika muonekano mpya ambao haujawahi kutokea katika video nyingi za wasanii wa kibongo.

Msanii huyo hasa ujio wa video hiyo ndipo alipozungumzia kuwa imeshakamilika na kinachosubiriwa ni kuitoa na mashabiki waweze kuona kilichofanyika.

Izoo alisema kuwa anaamini kazi yake iko poa hivyo hana wasiwasi sokoni kwani kila kazi anayotoa inakubalika ingawa wimbi la wasanii linampa changamoto ya kufanya kazi nzuri ambayo itaendelea kumpa heshima kutokana na jina lake.

“Video yangu inakuja nadhani Ijumaa hii inayokuja hivyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani kitu kimetulia, kama wanavyojua mara zote huwa nafanya kazi ambazo mashabiki wangu wakisikiliza wanapata mzuka kutokana na mashairi na hata mtiririko wa ngoma njisi ulivyopangwa,” alisema.

Views: 127

Tags: B, HII, IJUMAA, IZZO, KIDEONI

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by Calvin Wilbert on September 26, 2012 at 1:47pm

much respect brodahh!!


 

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service