
Bosi wa kundi mahiri la muziki wa Hip hop hapa Bongo, lijulikanalo kama Kikosi cha Mizinga lenye maskani yake pande za Kinondoni jijini Dar, Kalama Masoud Kalapina amesema ujio wa nyota wa muziki huo kutoka Marekani Rick Ross kwenye tamasha la Fiesta 2012 ni zaidi ya shoo kwa wasanii wa Tanzania.
Akizungumza na teentz.com mapema leo Kalapina amesema kuwa wasanii wa Bongo hawataakiwi kwenda kwenye shoo ya fiesta kwa ajili ya kupiga picha na mkali huyo kwa ajili ya facebook na twitter ama kwenda kugusa tumbo kwani hazitawasaidia chochote kwenye muziki wao.
Hatutakiwi kwenda kwa ajiri ya facebook na twitter isipokuwa tunatakiwa kwenda kujifunza mbinu anazotumia kutawala jukwaa na pia kujaribu kuzungumza naye kuhusu njia ambazo anatumia kupata mafanikio kimuziki na zaidi kipi kimemfanya kuwa mmoja ya mastaa walioleta mapinduzi kwenye muziki wa sasa alisema Kalapina.
Akiendelea zaidi Kalapina alisema kuwa ujio wa Ross ni kitu kikubwa sana kwenye muziki wetu wa Tanzania na kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza nchi yetu hivyo anatoa pongezi zote kwa kampuni ya Clouds Media kwa kufanikisha ujio huu.
Comment
Comment by Mkomwa Salum on October 12, 2012 at 1:19pm its true big bro umewachana afu inshu za playback hatuzimaind
Comment by emmanuel mushi on October 4, 2012 at 11:07am dats true ma bwoy kalapna coz most of artist wanazani kuwa iyo ndo day yakutuuzia sura instead of learning and imitiating
Comment by emmanuel mushi on October 4, 2012 at 11:05am dats true kalapina coz wasanii wetu wengi wanazani kuwa hiyo ndio siku ya kutuuzia sura
Comment by Innocent Quanama on October 2, 2012 at 3:53pm that's good kamanda Kala Pina,,,
Comment by innocent kowe on September 30, 2012 at 2:14am Hiphop staa wa Tanzania Albert Mangweha alifariki dunia akiwa Afrika Kusini May 28 2013 ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana na siku…
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ