
Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa Dar, hivi karibuni amejitokeza na kudai kuwa yeye ndiye mganga aliyempaisha mwanamuziki Nasibu Abdu ‘Diamond Platnumz’ ambaye kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.
MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA SUPASTAA
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa.
Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani alipokuwa akihangaika kuchomoka kisanii.
Mganga huyo alifunguka kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuchukuliwa na watu waliompeleka kwa waganga wa Kigoma ambako anajidanganya kuwa ndiyo wanampaisha kumbe walimchukua akiwa ameshampandisha kwa kumpa dawa kali za mvuto.
ALIMPA DAWA GANI?
Alizitaja dawa alizompatia Diamond kuwa ni mitishamba aina ya Dubi, Ntajamasala (hii humfanya watu wamuogope na kumheshimu), Italigula, Nkangacharo na Kalila Lila (ambayo huichoma na kuoga kwa ajili ya kuwavutia watu).
ANGUKO LA DIAMOND
Alidai kuwa Diamond amejisahau na hajui kama anguko lake linakuja kufuatia ahadi aliyoiweka wakati anaanza kuimba baada ya kumpatia dawa hivyo atapotea kwenye muziki.
Akielezea historia ya kukutana kwao, Ustadhi Yahya alisema yeye na staa huyo walikutana miaka ya 2000 nyumbani kwa Papaa Misifa ambaye alikuwa meneja wa Diamond.
Alidai kuwa kubadilika kwa Diamond kulikuja baada ya kutwaa tuzo tatu za Kili mwaka 2010 ndipo akawa anahusudu wanawake tofauti na masharti ya dawa japokuwa alimkanya lakini hakumsikia.
DIAMOND ANASEMAJE?
Kama ilivyo desturi ya gazeti hili, lilimgeukia Diamond ili kupata mzani wa habari hiyo ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa maelezo yake yote.
AMKANA
Katika maelezo yake, Diamond alikataa kata kata kuwa hamfahamu mtu huyo kisha akakata simu.
“Sina msikiti nitakuwaje na Ustadhi? Huyo mganga nasema simfahamu,” alisema kisha akakata simu.
source : GLOBAL PUBLISHERS WEBSITE
Comment
Comment by ISSABELA PATRICK on February 25, 2013 at 3:50pm lkn!ss watanzania bwana mtu asifanikiwe
Comment by sam juma on February 10, 2013 at 5:09pm hayo yote maneno ya mkosaj2
Comment by Peter frank on February 8, 2013 at 9:12pm uongo mtupu
Comment by Johnson Godfrey Chowa on February 6, 2013 at 10:03pm Au na story hii diamond anataka public attention mana kwa ku tunga vitu hawa masuparstar kawaida tu na kama huamini story hii itaishia hewani
Comment by james machim on February 4, 2013 at 9:17pm me siwezi kuwa na msimamao wa moja kwa moja ingawa mbea husema ukweli sema tu hajaruhusiwa....ila uchunguz ufanyike zaid huenda kuna ukweli ndani yake.
Comment by Msafiri Sanga on February 3, 2013 at 10:59am
Comment by ESSAU NGOBEI on February 3, 2013 at 9:30am mganga amebandika matangazo bado amekosa wateja sasa amebuni mbinu nyingine ili wanaoanza mziki wamtafute.....kweli hii ni bongo dar es salaaaaammmmmm
Comment by vintan gabriel kantinga on February 3, 2013 at 8:59am
Comment by Mzee Shaban on February 2, 2013 at 7:15pm Added by tanjin tareq on May 18, 2013
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ