
Kupitia teentz pekee ngoma mpya ya mkali aliyewahi kutamba na singo ya sikati tamaa Darasa iko kwa hewa,ambapo unaweza kuisikiliza na kujua kile kipya ambacho mkali huyu amekuja nacho,katika mazungumzo yake mafupi na mtandao huu namba moja kwa habari za burudani hapa bongo jamaa alifunguka yafuatayo
"Plan zangu ni kutimiza moja kati ya ndoto zangu, ambayo ni kuwa na album haijalishi inalipa au hailipi kiasi gani nilishasema neno hilo miaka mingi iliyopita. Nilikua nanunua album ya machozi jasho na damu so najidai na album ikiwa ngoma itaenda vizuri inshaalah. Pia movie ya sikati tamaa kama mungu akipenda itakua mtaani soon ambayo inaeleza maisha na hustle zangu, na ndani wako watu kama Dj Choka, Madee, Godzilla, Adam Mchomvu, Ze boy na wengine wengi wakiwemo bongo movies na mimi nikiwa kama muhusika mkuu" amesema Darasa
Comment
Comment by Paul Charlee on October 16, 2012 at 5:36pm Added by jenry jeny on May 17, 2013
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ