TEEN TZ

WAKALI muziki wa  kizazi kipya  Bongo Ramadhani Kalesela 'Pingu' na Deogratius Freddy 'Desso' ambao kitambo kidogo walitengana na  kufanya kazi ya muziki wakiwa pande mbili tofauti  kutokana na  sababu za hapa na pale wamerudi  kufanya  kazi pamoja  kama ilivyokuwa awali.

Akipiga  stori na  Teentz.com mapema leo Bosi wa  Kruu ya 'Tip Top Connection', Bab Tale, ambaye ndiye amesimamia mpango mzima  wa nyota hao kutoka  upya wakiwa pamoja amearifu kuwa mara  kadhaa alikuwa  akipata maombi kutoka kwa  mashabiki wa muziki wa  kizazi kipya  juu ya  kuwaweka pamoja tena wakali hao hivyo akaona kuna haja ya kuheshimu mawazo  ya  mashabiki wake  na kuamua kuweka kando tofauti zilizokupo  na kuwatoa upya nyota hao kwenye ngoma mpya   iliyopewa jina  la  'Jicho Usimbanie'.

"Yalikuwa  ni maombi ya mashabiki, walitaka kusikia  ngoma  kutoka kwao wakiwa pamoja, nashukuru mungu kuwa nilipowaambia jambo hilo hawakuping ana hatimaye kazi imefanyika  kikubwa ni wadau kuipokea   ngom ahiyo ambayo rasmi itautambulisha uwepo wa pamoja tena kwa wasanii hao ambao kitambo waliowahi kutamba na ngoma ya 'Jonita'" alisema  Talle

kwa upande wake  Desso ameimabia  Teentz.com  kuwa alikuwa siku zote amekuwa akisubiri kwa shauku kubwa nafasi ya kufanya kazi akiwa pamoja na mshikaji wake huyo wa Long Time, hivyo anashukuru kuwa hilo limetimia katika wakati huu muhimu ambao muziki wa kizazi  kipya unazidi kusambaa duniani kote.

"siku zote  nimekuwa nasubiri kwa hamu nafasi hii nashukuru kuwa  ndoto imetimia  ninachoamini   ni kuwa  huu ni mwanzo wetu wa kufanya makubwa kwenye muziki huu  kama ilivyokuwa awali, nawashukuru mashabiki wetu kwa kutuvumilia na kuonyesha kuwa walimisi kazi zet ni wakati wao sasa kufurahiakile walichokuwa  wakikiomba kila siku" alisema.

 

 STORI NA DISMAS TEN 0718489260

Views: 255

Tags: DESSO, NA, PAMOJA, PINGU, TENA

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by Gwakisa David Mwaihabi on July 31, 2012 at 6:45pm

NIC BROTHERS

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service