
Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini, Afande Sele na 20 Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja kwa nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.
Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele kuzungumza na Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20 Percent cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa amelipwa pesa zote.
Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii huyo na kubaki na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao shilingi milioni moja waliyompa kwa ajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.
Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio kuhusiana na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.
Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni kama ‘mtoto’ na alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila kujuwa sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.
Juzi kati kupitia ukurasa waFacebook Afande Sele alicaharanga walaka ufuatao:
“Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twenty Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugumu, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mmefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)
BY DISMAS TEN 0718489260
Comment
Comment by Tumaini Chanyika on July 23, 2012 at 9:53pm 'non are right'
Comment by Gullam Mohammed Rashid on July 21, 2012 at 2:37am dogo ananata sasa ila king mi nakupa big up mpe darasa kijana asidharau mikataba bana kwani alikuwa wapi alipo sign?
Comment by Rashid Shomar on July 17, 2012 at 11:46am Hivi tuna jifunza nin?kama wakubwa ndio ambao wanatakiwa kuelewa kwamba mdogo wangu ana kasoro gan na anahitaj nin katka maisha nakutupa muongozo mzur na baadala yake wamekuwa ni watu wenye wivu na maisha ya wadogo zao,kwa hali hii taifa.Lita rise up.na je ana mpango gan na ndugu yake huyo ,maana tunapenda mtu akikosa anarekebishwa anakili.na pia tunakua naye katika kujenga taifa na mara nyingi kila anaye ulizwa anasababu zake,Na kabla ya swali kunakuwa na jibu ili ukikosea unarekebishwa.kwa mi binafsi huwa nakosa raha sana raster wakitofautiana maana daima niwatu wakuelewana na we 20paa tupe sababu ili tuweze kuweka sawa wanyonyaji.Na pia huwezi kuajiri mtu na kumpa kaz mbali na alipo ajitegemee mwenyewe ukabaila uu.
Comment by ibrahim juma on July 16, 2012 at 9:05pm 20 pa is a damn bustard!!hawez kutumia lugha ya nmna ile kwa redio!!hey bro r yu f***** up!!
Comment by Steve Mpepo on July 16, 2012 at 1:16pm so sorry broo!!! ila bado unanafasi ya kukaa nae ukamweleza hyo mambo isiwafanye mkatofautiana, ni hayoo 2!!!!
livehoba posted a status
livehoba posted a status
Godfrey Solomon commented on Teen Newz's blog post HII INAWEZA KUWA NDIYO REASON KWA NINI OBAMA HATOENDA KENYAAdded by tanjin tareq on May 18, 2013
© 2013 Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.
You need to be a member of TEEN TZ to add comments!
Join TEEN TZ