TEEN TZ

DOGO JANJA ATUPIWA VIRAGO TIP TOP CONNECTION

Nyota wa muziki wa kizazi kipya  kutoka  ‘kruu’ ya  Tip Top Connection  yenye maskani yake pande za  Manzese  jijini  Dar  es  Salaam  Abdul Abubakar Chende  ‘Dogo  Janja’  ametupiwa  virago   ndani ya kundi hilo.

Akizumngumza na  Teentz .com mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally  ‘Madii’  amesema kuwa  Dogo Janja  ameshindwa  kuendana na  makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo  kuhudhuria  shuleni kama alivyokuwa akitakiwa  kufanya kila siku  badala yake  amekuwa akiendekeza  starehe na  wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.

“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa  maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya  kurudi kwao  na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake  kumuarifu kuwa Tip Top   hatuko na mwanae kwa sasa”  alisema Madii

Katika hatua nyingine Madii  amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na  kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi  kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa  na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega shule na kwenda kujificha  nyumbani kwa TundaMan  hukua akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.

Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na mara moja  kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda  kumsaka,  lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha  uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya  alikanyaga  kuku  na  siri yake kujulikana kuwa amejificha hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho chake  tayari kurejea ‘kileji’.

"vimekuwa ni vitendo vya kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'

 

                                               ….Stori by  Dismas Ten……   

Views: 2305

Tags: ATUPIWA, CONNECTION, DOGO, JANJA, TIP, TOP, VIRAGO

Comment

You need to be a member of TEEN TZ to add comments!

Join TEEN TZ

Comment by Edwin Gailanga on June 26, 2012 at 12:06am
aaaaaa hi ni kwli? dogo ameanza kuyaona Mara hii? bt tiptop watambue tatizo co kulikimbia Bali kukabiliana nalo huyo bado dogo n kukachin na kumweleza 2.
Comment by angela sijale on June 17, 2012 at 2:36am

na huo umri wake ni starehe gani aliokua akiifanya huyu mtoto..!!! ka

???

Comment by Pancras Suday on June 16, 2012 at 10:08pm

Duh! acha atangulie kileji, shule muhimu bhana inakuuwaje dogo anatega shule

Comment by jonawyne on June 16, 2012 at 6:21pm

safiii ndi dawaaa

Comment by raphael bihemo on June 16, 2012 at 4:39pm

Advice kwa dogo janja popote alipo, keshakanyaga kinyesi, hawezi kuukata mguu bali kuusafisha na kuwa makini, shule kwanza starehe baadae. dat wat's up.

Comment by Praygod Fadhili on June 16, 2012 at 12:10pm
Dogo amelewa sifa. Alikuwa anataka kufanya ya Mr Blue
Comment by win paul on June 15, 2012 at 3:07am

Dah madee a tink twic bwana,,,so sry 4 dogo janj 

bt ac gvup bhana w stil nid him in d' game

Comment by Successor Dér Führer on June 13, 2012 at 10:23pm

Akajifunze kwanza tabia na kuishi powa na watu, ajue umaarufu ni mzigo wa miba ukiubeba unaumia.

Comment by dennis mrosso on June 13, 2012 at 9:25pm
lakin mazee kama ndo kosa la kwanza c anasamehewa na kama ni xul c anaendelea kama kawa wakubwa!!! Mi naona hiyo kumtoa kwenye ku
ndi so solution ya kumsaidia.....!!!!!
Comment by Bragatwice on June 13, 2012 at 7:56pm
Maamuzi walofanya tip top xo mabaya bt m2 akikosea c anarekebshwa kwanza

G5 CLICK - LATEST NEWS

Advertisement


 

© 2013   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service